Jumapili, 31 Mei 2015

MH.MWIGULU ALIVYOTANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS MKOANI DODOMA JIONI YA LEO

  Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akiwapungia mkono baadhi ya wafuasi wake waliojitokeza kwa wingi,kumsikiliza wakati akitamka kutangania nia ya kugombea kiti cha uraui kupitia CCM


  Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakimsikiliza kwa makini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea kiti cha Urais kupitia chama cha CCM
 Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Dodom mapema jioni ya leo katika moja ya ukumbi wa chuo cha Mipango
Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakimsikiliza kwa makini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea kiti cha Urais kupitia chama cha CCM
TAASISI YA MISA YAWANOA WAANDISHI WA HABARI NJOMBE KUHUSU MATUMIZI YA INTANETI


Mwenyekiti wa MISA, Simon Berege akitoa mafunzo kwa wanahabari mkoani Njombe kuhusu matumizi ya Intaneti yaliyofanyika Altek mjini Njombe





Mercy Sekabogo mwandishi wa habari akiwa katika mafunzo ya mtandao yaliyotolewa na MISA mjini Njombe


Na Mwandishi Wetu, Njombe

Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika (MISA) imetoa mafunzo ya siku nne kwa waandishi wa habari mkoani Njombe, lengo likiwa ni kuwafundisha kujua jinsi ya kutumia Intaneti.

Mafunzo hayo yanatolewa na Mwenyekiti wa Misa, Simon Berege kwa kushirikiana na Kaimu Mkurugenzi, Andrew Marawiti yakiwashirikisha waandishi wa habari wa kujitegemea pamoja na watangazaji wa redio na Luninga.

Akitoa mafunzo hayo, Berege aliwaasa waandishi hao wa habari kutoka wilaya ya Makete, Ludewa, Halmashauri ya Mji Makambako na mjini Njombe kujifunza kutumia mtandao wa Intaneti kama sehemu mojawapo ya kuweza kutafiti mambo mbalimbali katika habari wanazoziandika.

Mafunzo hayo ya MISA yanatolewa kwa lugha ya kiswahili  tofauti na miaka mitatu iliyopita ambapo yalitolewa kwa lugha ya kiingereza, kusudi limekuwa ni kuwafanya waandishi wengi kuielewa vyema lugha ya kiswahili.

Vilevile mafunzo yamelenga kuwataka wanahabari hao kutumia  Intaneti kwa ajili ya  kufanya utafiti wa habari mbalimbali kupitia mtandao ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu vijijini.

Mbali na hilo, pia wanahabari wanatakiwa kujifunza umuhimu wa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari katika kutumia Intaneti.
Aidha wanahabari hao wanatakiwa kuzingatia usalama wa teknolojia ya habari na umuhimu wake. Kujua namna ya kutumia mitandao ya kijamii na umuhimu wake kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani nchini.

MWIGULU NCHEMBA KUTANGAZA NIA YA URAIS ALASIRI YA LEO



Interested Advertising Mwigulu Kugommbea Nchemba Presidency today at 9 afternoon.

As usual, the search will be aired to give you the key points of his policy.

EDWARD LOWASSA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA TANZANIA, JIJINI ARUSHA LEO

 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SOURCE:http://issamichuzi.blogspot.com/
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
 Mh. Lowassa akiwapungia wananchi.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo,  kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa wakati wa mkutano uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Mh. Edward Lowassa akipongezwa na baadhi ya Wabunge waliohudhulia mkutano huo, baada hotuba yake.

PITIA VICHWA VYA MAGAZETI-MEI 31,2015

12
5
6
8
7
10
9
34

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MAALIM SEIF IKULU DAR ES SALAAM

2

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad ikulu jijini Dar es Salaam
(picha na Freddy Maro)

1

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad ikulu jijini Dar es Salaam.